BAKWATA: Kifungu kinachoruhusu mtoto wa miaka 14 kuolewa kisiondolewe

0
21

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limependekeza kifungu cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kinachoruhusu msichana wa umri wa miaka 14 kuolewa kwa amri ya mahakama kisiondolewe.

Akitoa maoni hayo Mwanasheria Mkuu wa BAKWATA, Hassan Fatihu alipowasilisha mapendekezo kwa Tume ya Kuangalia Jinsi ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini amesema sheria ya ndoa ibaki vilevile kutokana na ukinzani uliopo kati ya sheria ndoa na sheria ya mtoto pamoja na imani za dini.

“Sisi Waislamu tunaamini mtoto wa kike akishavunja ungo anaruhusiwa kuolewa, nami naruhusiwa kuoa haijalishi nina miaka 10, 12 au 13,” ameeleza Fatihu.

Nchi 10 za Afrika ambazo watu wake wana furaha zaidi

Ameongeza kuwa sheria ya mtoto inaeleza kuwa mtu yeyote aliye chini ya miaka 18 ni mtoto, na kwamba sheria ya ndoa imeruhusu mtoto kuanzia umri wa miaka 14 kuolewa kwa ridhaa ya mahakama ambapo itaangalia vitu vingi ili kuruhusu ndoa hiyo ikiwa ni pamoja na afya ya mtoto, mila na tamaduni za jamii husika.

Chanzo: Habari Leo

Send this to a friend