Rais abaini wanaostaafu/kutenguliwa kuondoka na mashine za kukusanya fedha
Rais Samia Suluhu Hassan amekemea tabia ya baadhi ya wafanyakazi kutoka halmashauri wanaostaafu au kutenguliwa kazini kuondoka na mashine zinazotumika katika ukusanyaji wa fedha (POS) na kusababisha ukusanyaji wa fedha kutofanyika vizuri.
Ameyasema hayo wakati akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/2022 pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Ikulu jijini Dar es Salaam.
“Mtu kama ameondoka kazini kwa kustaafu, ameondoka kazini ametenguliwa anaondoka na hicho kimashine cha POS, kwa hiyo halmashauri inakusanya wanavyoona ukiwauliza wanasema POS ameondoka nayo fulani. Sasa huu mfumo ambao mtu anaweza kuondoka nayo ikawa haki yake, ebu itazameni vizuri,” amesema.
Rais Samia aitega wizara ya kilimo kuhusu fedha alizotoa
Aidha, Rais Samia amezitaka taasisi za Serikali kuwa na nidhamu ya kazi na kuonesha mfano kwa sekta binafsi katika ulipaji wa kodi pamoja na kuomba risiti pindi zinapofanya manunuzi mbalimbali.
Mbali na hayo ameitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuangalia namna ya kufanya kazi na sekta binafsi hasa katika uimarishaji wa mifumo pamoja na uhamilishaji wa teknojia ili kuipunguzia gharama Seriakali za kununua vifaa vya bandari.
“Hakuna sekta binafsi ataweka pesa yake pale akubali mifumo ibakie hivi ataimarisha isomeke vizuri na fedha ikusanywe,” ameeleza