Waziri Nape: Niliambiwa nikichunguza uvamizi Clouds nitafukuzwa kazi

0
27

Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema aliamua kuchagua heshima badala ya cheo chake wakati wa uchunguzi wa sakata la uvamizi wa kituo cha habari cha Clouds Media Group uliodaiwa kufanywa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mwaka 2017.

Akisimulia kisa hicho, Nape ambaye wakati huo alikuwa akihudumu kama Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema wakati alipounda tume ya uchunguzi ndani ya saa 24 kuchunguza tukio hilo, alizuiwa kufanya uchunguzi huo na kuambiwa kuchagua kati ya kuachana na uchunguzi au kufukuzwa kazi.

“Asubuhi yake nilizuiwa kwenda kuchunguza nikaambiwa ukienda utakuwa hauna kazi, nikasema ni bora nisiwe na kazi lakini nilinde heshima yangu,” amesema.

TCRA yavionya vyombo vya habari kuhusu taarifa za kidini za kufikirika

Ameongeza, “kwa sababu katika mazingira wewe ndiye waziri, watu wanavamia kituo halafu wewe unatakiwa usiende, unachagua kati ya heshima na kazi, heshima utaenda nayo, kazi ipo siku itaondoka tu. Kwa hiyo nikachagua heshima ambayo ndiyo nadhani naendelea nayo leo.”

Hata hivyo, baada ya uamuzi wake wa kuchagua kuendelea na mkakati huo alitenguliwa katika nafasi yake siku moja baada ya kupokea ripoti ya kamati ya uchunguzi na aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Magufuli.

Send this to a friend