Bilioni 8 zatengwa kusomesha madaktari bingwa 400

0
20

Serikali imetenga zaidi ya TZS bilioni 8 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa “Samia Suluhu Super Specialists Programe” itakayosomesha madaktari bingwa zaidi ya 400 ndani na nje ya nchi.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema mkakati huo unalenga kusomesha wataalamu kwa mfumo wa kujiendeleza katika fani za kibingwa, na wanapomaliza wanarudi katika vituo vyao ili kuendelea na majukumu yao ya kuwahudumia wananchi.

Ameongeza kuwa utaratibu huo utaosomesha wataalamu kwa muundo wa jumuhishi yaani daktari bingwa, muuguzi, mtu wa usingizi.

Mkurugenzi aliyedaiwa kuuza viwanja kwa bilioni 1 atumbuliwa

Aidha, Waziri Ummy amesema Wizara imepata kibali kipya cha ajira, hivyo imelenga kuajiri madaktari bingwa na kuwasambaza katika hospitali za Rufaa za mikoa hasa zile zenye changamoto ya upungufu wa madaktari ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Naye, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel akijibu juu ya uhaba wa madaktari bingwa katika hospitali ya Kitete Tabora, amesema Wizara imepeleka kusoma jumla ya madaktari sita kutoka hospitali hiyo ambapo madaktari wawili wanasomea ubingwa wa magonjwa ya ndani, daktari wa magonjwa ya Kinywa, Sikio na Koo, daktari bingwa katika Mionzi, daktari bingwa katika magonjwa ya dharura, na daktari bingwa wa Afya ya akina mama na uzazi.

Send this to a friend