Kenya: Waislamu wailaumu Serikali kuwapotosha kusherehekea Eid Ijumaa  

0
25

Baadhi ya Waislamu nchini Kenya wameishutumu serikali ya Kenya kwa kuwapotosha watu baada ya kutangaza kuwa Ijumaa ni siku ya mapumziko kwa ajili ya Eid al-Fitr.

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya, Kithure Kindiki alitangaza siku ya Jumatano kwamba Ijumaa ni siku ya mapumziko kwa ajili ya Eid.

Yemen: Watu 78 wafariki wakipatiwa msaada wa Ramadhan 

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu nchini Kenya (Supkem), Hassan Ole Naado, ambaye alizungumza na gazeti la Nation, amesema  tangazo la serikali limewapotosha Waislamu nchini humo, kwani uamuzi wa siku ya Eid hutegemea kuandama kwa mwezi.

“Serikali inafaa kuomba ushauri Waislamu kabla ya kufanya uamuzi. Hili ni kosa kubwa na upotoshaji,” amesema.

Hata hivyo baadhi ya Waislamu nchini humo wameandika kwenye mitandao ya kijamii wakilaani hatua ya serikali.

Send this to a friend