Mufti aomba Serikali na wadau kununua chombo cha kutazamia mwezi  

0
26

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir ameiomba Serikali na wadau kusaidia upatikanaji wa darubini ya kukusanya taarifa za mwandamo wa mwezi (moon sighting machine) ili kuimarisha uhakika wa taarifa.

Ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 22, 2023 katika swala ya Eid El- Fitr iliyofanyika kitaifa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI uliopo Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam ambapo imehudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mabalozi, mawaziri na waumini wengine.

 “Tunashukuru mabalozi, mawaziri na watu wenye uwezo mliopo hapa, kuna chombo tunakihitaji cha kutazamia mwezi. Wenzetu Kenya na Zanzibar wanavyo vifaa hivi, kwa hiyo na sisi tunaomba juu ya jambo hili mtusaidie kunyoosha mkono ili kufanikisha,” amesema Mufti.

Kwa mujibu wa BAKWATA, Tanzania kupitia Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  imekuwa ikikusanya taarifa hizo kwa kushirikiana na mataifa ya Kenya na Zanzibar zinazoendana pia na taarifa za Saudia Arabia na mataifa mengineyo duniani.

Send this to a friend