IMF yaidhinisha mkopo wa TZS bilioni 358 kwa Tanzania

0
27

Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeridhia kuikopesha Tanzania dola 153 milioni (TZS bilioni 358.9) kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa bajeti yake.

Shirika hilo kupitia kwenye tovuti yake imeeleza kuwa fedha hizo zinafanya jumla ya mkopo kufikia dola milioni 305 (TZS bilioni 715.5) kati ya dola bilioni 1.04 (TZS trilioni 2.4) zilizoidhinishwa kwa Tanzania mwaka huu.

“Licha ya kuwepo kwa changamoto za kiuchumi duniani lakini Tanzania inachukua hatua nzuri kwenye eneo hilo, mamlaka zinapaswa kufanya kazi ili kuongeza mapato ya ndani, kupunguza urasimu na kukabiliana na rushwa,” imeeleza IMF.

Serikali yapiga marufuku matumizi ya vyandarua kwenye bustani za mboga

Hata hivyo, IMF imetoa angalizo kwa Tanzania kuimarisha usimamizi wa fedha kwa kuboresha ufanisi wa matumizi ya fedha na kukwepa malimbikizo ya madeni ya ndani huku ikiitaka kuongeza mapato ya ndani kwa ajili ya kujiimarisha zaidi kiuchumi.

Naye, Mkurugenzi Msaidizi wa IMF, Antoinette Sayeh amesema kwa sasa deni la Tanzania bado ni himilivu na la wastani, hivyo ni muhimu kuendelea kuweka kipaumbele katika mikopo yenye riba nafuu.

Send this to a friend