Wanafunzi asilimia 97 wafeli mtihani Shule Kuu ya Sheria

0
31

Matokeo ya mtihani wa Uwakili kwa wanafunzi wa Shule Kuu ya Sheria (LST) nchini yameendelea kuwa changamoto baada ya wanafunzi 23 pekee kufaulu kati ya wanafunzi 821, yanayohusisha wanafunzi wa kipindi cha masomo Januari hadi Desemba mwaka jana.

Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Mwananchi, matokeo hayo yaliyotoka Aprili mwaka huu ambapo wanafunzi 497 wanatakiwa kurudia baadhi ya masomo, huku wanafunzi 301 wakikatishwa masomo yao.

Asilimia 96 ya waliofanya mtihani Shule Kuu ya Sheria mwaka 2022 hawajafaulu

Miezi sita iliyopita, Serikali kupitia Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro aliunda kamati ya kuchunguza na kutoa mapendekezo yenye wajumbe saba ili kutafuta chanzo cha kufeli kwa wanafunzi wengi kwenye mitihani hiyo ya mwisho inayowapa sifa ya kuwa mawakili.

Katika matokeo ya mwaka 2022 muhula wa 33, yalionesha wanafunzi 26 (sawa na asilimia 4.1) ndiyo walifaulu huku wanafunzi 342 wakitakiwa kurudia baadhi ya masomo na wanafunzi 265 (sawa na asilimia 41.9) wakifeli na kukatishwa masomo yao.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend