Mkuu wa kikosi cha usaidizi cha RSF, Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, anayefahamika zaidi kama Hemedti amesema hatofanya mazungumzo mpaka mashambulio ya mabomu yatakapomalizika.
Akizungumza na BBC, Hemedti amesema kuwa wapiganaji wake wanaendelea kupigwa mabomu tangu makubaliano ya siku tatu ya kusitisha mapigano, hivyo atazungumza ikiwa usitishwaji wa mabomu utaheshimiwa. Baada ya hapo tunaweza kuwa na mazungumzo,” amesema.
Wanadiplomasia na raia wa kigeni waendelea kuikimbia Sudan
Kiongozi huyo amesema hawana lengo la kuiangamiza nchi hiyo huku akimtupia lawama zote mkuu wa majeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan kwa machafuko hayo.
Hededti amesema hana tatizo la kibinafsi na Jenerali, lakini anamchukulia kama msaliti kwa kuwaleta ndani ya serikali wale waliokuwa watiifu kwa rais wa zamani Omar al-Bashir, ambaye alipinduliwa na jeshi na RSF pamoja mwaka 2019 baada ya maandamano makubwa.