Serikali imesema hadi sasa, jumla ya watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Marburg ni tisa ambapo kati ya hao watatu wamepona akiwemo daktari aliyewahudumia wagonjwa wa mwanzo kabla ya kuthibitika, huku wagonjwa sita wakipoteza maisha akiwemo mtumishi mmoja wa afya na mtoto wa miezi 18.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Afya imesema kuanzia Aprili 21 mwaka huu hakuna mgonjwa yeyote aliyegundulika kuwa na virusi vya ugonjwa huo mkoani Kagera.
Tiba 5 za asili za magonjwa mbalimbali unazoweza kuandaa nyumbani
“Wagonjwa wawili waliokuwa wamesalia katika vituo maalum vya matibabu waliruhusiwa kutoka tarehe 20 na tarehe 21 Aprili, 2023 baada ya kuthibitika kimaabara kuwa hawana tena virusi vya Marburg,” amesema Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
Aidha, amesema watu 211 kati ya 212 waliokuwa wametengamana na wagonjwa na kuwekwa karantini wameruhusiwa baada ya kumaliza siku 21 za ufuatiliaji bila kuonesha dalili za ugonjwa huo, hivyo ni ishara kuwa jitihada za pamoja zilizofanyika katika kukabiliana na mlipuko huu zimeleta mafanikio makubwa.