Watoto 900, wajawazito 57 wafariki kwa kukosa huduma za uzazi

0
33

Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigela amesema zaidi ya watoto 900 na wajawazito zaidi ya 57 mkoani humo wamefariki kwa kukosa huduma za awali za uzazi, wakati wanajifungua katika maeneo yao kwa mwaka 2022.

Amesema ukosefu wa huduma umekuwa tishio kwa akina mama wanaojifungua mkoani humo, hivyo imeilazimu Wizara ya Afya kuja na mpango mpya unaojulikana kwa jina la ‘M-Mama’ utakaowawezesha wajawazito kuhudumiwa na magari maalumu katika maeneo yao ili kuondoa hofu na kupunguza vifo hivyo.

Watu sita wafariki kutokana na virusi vya marburg mkoani Kagera

“Zaidi ya watoto 900 walipoteza maisha ni namba kubwa, ni jambo ambalo halikubaliki na Serikali ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ni jambo ambalo analiwekea mkazo na hataki kuliona likitokea kwenye mkoa wetu,” amesema.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita, Omary Sukari amesema zaidi ya wanawake 120,000 hujifungua kwa mwaka mkoani humo huku akitaja moja ya changamoto kubwa zinazowakabili ni umbali wa kuzifikia huduma za afya.

Send this to a friend