Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesogeza mbele mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) kati ya Singida Big Stars dhidi ya Yanga SC uliopanga kuchezwa Mei 07, mwaka huu mpaka hapo utakapopangiwa tarehe nyingine.
Mabadiliko hayo ni kufuatia ombi la Yanga SC kuomba kupata muda zaidi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini utakaochezwa Mei 10, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Orodha ya wasanii 10 Afrika wanaotazamwa zaidi Youtube
Aidha, TFF imesogeza mbele mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam FC dhidi ya Simba SC uliopangwa kuchezwa Mei 06, mwaka huu katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na kupelekwa hadi Mei 07, mwaka huu.
TFF imesema mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa timu ya Azam FC na Simba SC kupata muda zaidi wa maandalizi kuelekea katika mchezo huo.