Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yaanza kutumika nchini

0
27

Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametangaza kuwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2023 iliyosainiwa na Rais Samia Suluhu Hassan Januari 31, 2023 imeanza kutumika kuanzia Mei Mosi mwaka huu.

Sheria hiyo iliyopigiwa chapuo na wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu imeanzisha vitu vitatu ambavyo ni Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, bodi ya masuala ya taarifa binafsi na ulinzi wa faragha ya watu.

Ajira milioni 14 kutoweka ndani ya miaka mitano ijayo

Akizungumza na wandishi wa Habari, wakili Benedict Ishabakaki amesema sheria hiyo inalazimisha wakusanya taarifa wote yakiwemo makampuni ya simu, hospitali, vyuo vikuu n.k kusajiliwa na tume ya ulinzi wa taarifa binafsi.

“Lazima uende ujisalimishe kwamba mimi ni mmoja wa wakusanya taarifa za watu ili uweze kusajiliwa. [..] Kwa sheria hii sasa imenyima kutoa taarifa za Mtanzania yoyote nje ya nchi bila aidha ya ridhaa ya tume ama bila ya ridhaa ya mtu husika,” amesema.

Send this to a friend