Mazoea haya ya kila siku yanaweza kuharibu figo zako

0
23

Ikiwa unataka kuishi maisha marefu, yenye afya, unahitaji kutunza figo yako. Lakini mazoea yetu ya kila siku yanaweza kuwa yanatuzuia kufanya hivyo.

Mabadiliko rahisi katika lishe yako, virutubisho, na usingizi utazuia ugonjwa wa figo katika siku zijazo. Kwa ajili ya figo zako, fikiria kubadilisha tabia hizi za kila siku.

Punguza chumvi nyingi
Wataalamu wanapendekeza watu wapunguze ulaji wao wa chumvi hadi kijiko kidogo kimoja cha chai kwa siku, au miligramu 2,300.

Pumguza matumizi ya dawa za kutuliza maumivu
Dawa za kutuliza maumivu hupunguza mtiririko wa damu kwenye figo zako. Baada ya muda, hii inaweza kusababisha figo kupata matatizo makubwa.

Jitibu Unapoumwa
Usipuuze magonjwa madogo madogo unapoumwa. Kuwa mwangalifu sana dhidi ya maambukizo ya bakteria kama vile strep throat na maambukizo ya sikio, kwa sababu yana hatari kubwa zaidi ya kuchuja figo zako.

Usibane mkojo
Kubana mkojo ndio sababu kuu ya shida za figo. Kadiri mkojo huo ukikaa mwilini mwako, ndivyo bakteria inavyozalisha zaidi. Bakteria wanaposafiri kwenye figo zako, uko hatarini.

Punguza vyakula vilivyosindikwa
Vyakula vilivyotengenezwa au vya kopo mara nyingi huwa na kiasi kikubwa cha sodiamu, ambayo itaharibu figo zako.

Aina 5 za vyakula ambavyo vikichanganywa hugeuka sumu

Punguza unywaji wa Soda
Unywaji wa soda mbili au zaidi kwa siku huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa figo maradufu. watafiti walibaini kuwa cola huongeza hatari ya figo kwa sababu ya asidi yake ya fosforasi.

Unafanya mazoezi ipasavyo?
Mazoezi hupunguza shinikizo la damu, huboresha usingizi, na kuimarisha utendaji wa misuli. Mazoezi hupunguza hatari zote kuu za ugonjwa wa figo.

Punguza vinywaji vya ‘Energy’
Kafeini kupita kiasi inayotokana na vinywaji vya kuongeza nguvu hasa kwa watoto, husababisha shinikizo la damu na mfadhaiko, ambayo yote husababisha uharibifu wa figo.

Unakunywa maji ya kutosha?
Vijiwe vingi kwenye figo hutokana na upungufu wa maji mwilini. Unapopungukiwa maji, mkojo wako unaweka mkusanyiko mwingi wa madini. Madini haya yanaweza kutengeneza fuwele ndani ya figo yako ambayo hukua na kuwa mawe.

Unapochelewa kuamka figo zako huzidiwa kazi
Watafiti wa Figo wanaeleza kwamba unapochelewa kulala, figo zako huendelea kufanya kazi kwa bidii. Unapaswa kulala saa saba mpaka tisa kila usiku.

Usitumie Dawa za Kujenga Mwili
Watafiti waligundua kuwa wajenzi wa miili tisa kati ya kumi walipata kovu kwenye figo kutokana na dawa za kujenga mwili.

Send this to a friend