China yapunguza mikopo kwa Kenya

0
29

Mikopo ya China kwa bajeti ya Serikali ya Kenya itakuwa ndogo zaidi katika kipindi cha miaka 16 huku Beijing ikichukua tahadhari zaidi katika utoaji wa mikopo barani Afrika ambapo baadhi ya mataifa yamefikia kikomo cha uwezo wao wa kukopa na mengine kusuasua kulipa.

Hati za hazina zilizotangazwa hadharani Jumanne zinaonesha kuwa ufadhili wa China kwa mwaka unaoanza Julai utashuka hadi Ksh1.74 bilioni [TZS bilioni 30] kutoka Ksh29.5 bilioni [TZS bilioni 508.7] katika mwaka huu wa fedha na Ksh71.2 [TZS trilioni 1.2] kwa mwaka wa 2017 .

Tangu Rais Ruto alipoingia madarakani Septemba 2022, ameahidi kupunguza kiwango chake cha kukopa, huku mikopo ya nje iliyotolewa kwa bajeti mpya ikishuka hadi Ksh313.8 bilioni [TZS trilioni 5.4] kutoka Ksh326 bilioni [TZS trilioni 5.6].

Nchi 10 zinazodaiwa zaidi na China

Kupungua kwa mikopo ya China kunaibuka katika kipindi ambacho Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeongeza kasi ya kutoa mikopo kwa nchi ya Kenya.

China imekuwa nchi inayokopesha Kenya kwa wingi zaidi tangu mwaka 2015 na kuiwezesha kutekeleza ujenzi wa miundombinu mikubwa, ikiwa ni pamoja na barabara na reli ya kisasa, ambazo imeinufaisha zaidi Nairobi katika miaka kumi iliyopita.

Send this to a friend