Uganda: Askari 10 wakamatwa kwa kuwaibia wezi

0
23

Maafisa 10 wa polisi waliokuwa katika kituo kimoja mjini Kampala nchini Uganda, wameshikiliwa baada ya majambazi waliowakamata kufungua jalada lao wakiwatuhumu askari hao kuiba nusu ya pesa walizoiba.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, wezi hao waliiba $110,000 [TZS milioni 260] na Euro700 [TZS milioni 1.9] kutoka kwa raia mmoja wa Burundi.

Baada ya tukio hilo wasamaria wema walisaidia kuwataarifu polisi kuhusu tukio hilo lakini inasemekena maafisa hao hawakuwaarifu wakuu wao kuhusu tukio hilo na kwenda kuwasaka wezi hao wakiwa peke yao.

Vioja: Wavunja duka na kuiba viatu 200 vyote mguu wa kulia

Inaelezwa kuwa baada ya maafisa kuwapata wezi hao wakiwa na kiasi hicho cha pesa, walitangaza kwamba walipata kiasi cha $20,000 [TZS milioni 47.1] na Euro500 [TZS milioni 1.3] pekee.

Hivyo, washukiwa ambao walikuwa wamekamatwa na kuzuiliwa, waliwaumbua maafisa hao na kueleza kwamba walitangaza chini ya nusu ya kile walichokuwa wamechukua kutoka kwenye maficho yao.

Maafisa hao walizuiliwa katika kituo cha polisi cha Katwe, sehemu ambayo wezi hao walikuwa wakizuiliwa kwa takriban saa 48 kabla ya kuachiliwa kwa dhamana wakisubiri uchunguzi.

“Nyumba za maafisa hao zitasakwa ili kurejesha kiasi cha pesa huku uchunguzi ukiendelea,” msemaji wa polisi amesema.

Send this to a friend