Lissu: Polisi hawajanikatalia kuchukua gari langu

0
21

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amepinga madai ya kuwa amekataa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kuhusu kushambuliwa na watu ambao hadi sasa hawajulikani na kueleza kwamba madai hayo hayana msingi wowote.

Akizungumza leo katika Ofisi ya Polisi mkoa wa Dodoma wakati alipofika kuliona gari hilo alilotumia wakati anashambuliwa mwezi Septemba mwaka 2017, amesema siku zote anataka tukio hilo lichunguzwe na yuko tayari kutoa ushahidi.

“Nimeiona gari kwa mara ya kwanza na ina matundu 30 ya risasi, imenipa shida sana kwa risasi zote zile zilielekezwa kwenye mwili wa mtu mmoja, nimeliona,” amesema.

Waziri Mkuu aagiza shule zifundishe zaidi kuhusu Mwalimu Nyerere

Aidha, amesema madai ya kwamba polisi wamekuwa wakiweka pingamizi la kulichukua gari hilo hayana ukweli wowote, hivyo atawasiliana na uongozi wa Jeshi la Polisi ili kulichukua gari hilo.

“Na kwa sababu kumekuwa na maneno maneno kuwa polisi wananikatalia kuchukua gari, naomba niseme wazi polisi hawajawahi kuwa na hilo wazo,” ameeleza.

Send this to a friend