Daktari aeleza tatizo la kupumua lilivyokatisha uhai wa Membe

0
24

Prof.Harun Nyagori ambaye ni Daktari wa Familia ya aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe amesema sababu iliyosababisha kifo cha mwanasiasa huyo ni maambukizi ya ghafla kwenye mfumo wa mapafu hewa (pulmonary embolism) na si kama inavyozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari, Dkt. Nyagori amewataka watu kuondoa mawazo potofu kuhusu kifo chake kwa kuwa ugonjwa uliomuua Membe ni wa kawaida na unaweza kumpata mtu yeyote.

“Tuondoe mawazo potofu ambayo yamekuwa yakizungumzwa mtandaoni kwamba aidha ameuawa au amepewa sumu na vitu kama hivyo, amekufa kifo cha kawaida ambacho mtu yoyote aidha mimi au wewe kinaweza kumpata,” amesema.

Wasifu wa Hayati Bernard Membe

Dkt. Haroun amesema Dkt. Membe amekuwa na afya njema katika miaka yote na hakuwahi kuwa na historia yoyote ya magonjwa sugu kama kisukari, magonjwa ya moyo, au presha.

“Jana alipata homa ndogo ya kifua, akipata shida ya kukohoa na kubanwa kifua na ilipofika usiku wa kuamkia alfajiri ya leo alishindwa kupumua ghafla akakimbizwa hospitali,” ameeleza.

Send this to a friend