Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imegharamia usafiri wa mashabiki 55 wa timu ya Yanga kwenda Afrika Kusini katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) dhidi ya Marumo Gallants.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Saidi Yakubu ikiwa ni hatua ya kuiunga mkono timu ya Yanga katika mchezo utakaochezwa Mei 17, 2023 kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng.
“Hii safari Serikali imesaidia Yanga kupeleka baadhi ya mashabiki 55 ambao wataondoka kesho Jumapili kueleka Afrika Kusini na huko wataungana na Watanzania waishio Afrika Kusini katika kuhakikisha wanatoa sapoti ya kutosha, nimeongea na Balozi na wao wamejiandaa kuwapokea kwa sababu pia wameandaa mabasi kutoka kila mji kuhakikisha Watanzania wanakuwa wengi,” amesema.
Ombi la Fei Toto lakataliwa tena TFF
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa timu ya Yanga, Andrew Ntime amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mchezo huo huku akitoa shukrani kwa Serikali kuwa mstari wa mbele katika kuiunga mkono timu hiyo ili iweze kufika fainali.