Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana amesema mgomo unaoendela kwa wafanyabiashara wa Soko hilo unasababishwa na kikundi cha watu wachache wenye maslahi yao binafsi.
Mbwana amesema kilio cha wafanyabiashara kilikuwa ni kusikilizwa na Rais Samia Suluhu Hassan, na katika kuonesha kuwa amewasikia alimtuma Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzungumza na wafanyabiashara sokoni hapo jana Mei 15, mwaka huu.
Waziri Mkuu: Rais Samia anataka kuona biashara zinafanywa kwa uhuru
“Alipokuja aliwaomba wafanyabiashara wafungue maduka na kuahidi kuwasiliza siku ya Jumatano. Nashangaa wafanyabiashara kuwa hawana imani na Waziri Mkuu,” amesema Mbwana.
Aidha, ameongeza kuwa ameomba msaada kwa vyombo vya usalama ili kuwachukulia hatua watu wachache wanaoonekana kunufaika na mgomo huo huku akieleza kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano.