Lifti ni salama sana, lakini kwa sababu ni mitambo kuna uwezekano kwamba ikatokea dharura za hapa na pale. Baadhi ya dharura huathiriwa na hali ya hewa na kukatika kwa umeme.
Bila kujali hali, lifti bado ziko salama hata kama zinasimama bila kutarajia au kukwama. Unapaswa kujua nini cha kufanya ikiwa utapata dharura ya lifti ili kuhakikisha kuwa haujihatarishi au kuhatarisha abiria wengine.
Kwanini watu huweka ‘airplane mode’ wakiwa ndani ya ndege
Mambo ya kuepuka unapotumia lifti;
1. Usitumie lifti ikiwa kengele ya tahadhari ya moto imelia, daima tumia ngazi ili uwe salama zaidi.
2. Usisimame karibu na mlango ili kuruhusu watu wengine kupanda kwa urahisi zaidi.
3. Usiingie kwenye lifti iliyojaa watu, subiri lifti inayofuata kwani inaweza kuwa imefika ukomo wa uwezo wake wa kubeba watu.
4. Usichezee kifaa chochote kwenye lifti, kusukumana, kupiga makelele, matusi, kuvuta sigara, n.k.
5. Usiegemee mlango wa lifti au kumsukumia mtu kwenye mlango.
6. Usiweke mkono wako kwenye mlango ili kuzuia mlango kufunga.
7. Usipande lifti iliyojaa watu ikiwa una mizigo mingi kuepuka kuwapa ghadhabu watu wengine.
8. Usitumie kitufe cha kufunga mlango ili kuzuia kumfungia mtu kwa bahati mbaya.
Mambo ya kuepuka inapotokea dharura ukiwa ndani ya lifti;
1. Usiogope ikiwa lifti itasimama katikati ya sakafu ‘floor’ au kukwama.
2. Usijaribu kupanda kutoka kwenye lifti iliyokwama isipokuwa kama milango imefunguka, na unaweza kuona kuwa uko salama kufanya hivyo.
4. Usiogope kwamba utaishiwa na hewa kwa sababu inazunguka na haitaisha.
5. Usiogope ikiwa hausikii mtu akijibu simu yako ya dharura kupitia mfumo wa lifti kwa sababu kuna mifumo ya mawasiliano ambayo hukuruhusu kuongea tu lakini haiwezi kujibu.
6. Usiruke Juu na chini. Wakati inapotokea dharura wengine hufikiria kuruka juu na chini kutaifanya ianze kufanya kazi tena lakini badala yake inaweza kuathiri mfumo na kufanya iwe vigumu zaidi kuokolewa..