Kufuatia taarifa iliyosambaa kwenye vyombo vya Habari ikimuonesha mtu aliyefahamika kwa jina la Baraka Mkama ambaye alitambulishwa kama wakili aliyekuwa akiwazuia askari wasiwatie nguvuni wateja wake baada ya kuachiwa huru na Mahakama, Baraza la Uongozi la Chama cha Sheria Tanganyika (TLS) limesema mhusika wa tukio hilo sio wakili wala mwanachama wa TLS.
Taarifa iliyotolewa na TLS imeeleza kuwa baada ya tukio hilo, baraza liliunda kamati teule ya uchunguzi wa tukio hilo na kufanikiwa kumhoji mhusika, Jeshi la Polisi, uongozi wa mahakama pamoja na baadhi ya mawakili waliokuwa na taarifa za tukio hilo.
Ufafanuzi wa Polisi kuhusu madai ya Kigwangalla kumpiga risasi mlinzi
“Katika mahojiano na kamati, Mkama alikiri kuwa yeye sio wakili ingawa amekuwa akifanya kazi kama wakili tangu mwaka 2019. Vilevile katika mashauri aliyokuwa anayasimamia akiigiza kama wakili, alikuwa akiwatoza wateja wake TZS milioni 3 na kuendelea kwa kesi,” amesema.
Aidha, TLS imesema itashirikiana na vyombo vya dola na vyombo vya utoaji haki ili kuhakikisha kuwa hatua stahiki za kisheria zinachukuliwa dhidi yake pamoja na watu wengine wenye tabia kama hiyo ambayo imekuwa ikienea maeneo mengi nchini.