Uingereza kuipa Tanzania msaada TZS bilioni 15

0
26

Tanzania imepokea msaada wa pauni milioni 5 sawa na takribani shilingi bilioni 15 kutoka Serikali ya Ungereza kwa ajili ya awamu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF).

Makabidhiano ya Hati za Makubaliano ya msaada huo yamefanyika jijini Dodoma kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Dkt. Mwamba amesema utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini Tanzania unaendelea vizuri jambo linalowezesha washirika wa maendeleo kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya mpango huo.

Naye, Balozi David Concar amesema Uingereza ni rafiki mkubwa wa Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo, hivyo nchi yake itaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha inatoa mchango wake katika kukabiliana na umasikini ili kuboresha hali ya maisha ya wananchi

Send this to a friend