Rais Samia aahidi kufanyia kazi ununuzi wa ndege nyingine ya mizigo

0
34

Rais Samia Suluhu ameahidi kufanyia kazi ombi lililotolewa na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kuongeza ndege moja kubwa ya mizigo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa pili wa miaka mitano wa Shirika hilo kwa mwaka wa Fedha 2022/23 hadi 2026/27 katika kukabiliana na hitaji la soko.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi ametoa ombi hilo wakati wa hafla ya kuipokea ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767-300F yenye uwezo wa kubeba tani 54 za mizigo, iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

Serikali yakanusha taarifa ya ndege ya Tanzania kusafirisha mizigo haramu

“Mmeomba ndege nyingine hapa ya mizigo, ahadi yangu kwenu wananchi, tutalifanyia kazi,” ameahidi Rais Samia.

Katika hotuba yake Matindi amesema mapokezi ya ndege hiyo yanaifanya ATCL kuwa na ndege 13 zilizopo na ndege 3 zinazoendelea kuundwa, huku ndege mbili kati ya tatu zikitarajiwa kuwasili nchini kati ya mwezi wa nane na mwezi wa 12 mwaka huu, na ndege ya tatu Boeing 787-8 ikitarajiwa kuwasili mapema 2024.

Aidha amesema kwa kutumia ndege za abiria kubeba mizigo, ATCL imeshika nafasi ya nne katika ubebaji mizigo ambapo ulinganifu huo umehusisha baadhi ya mashirika makubwa kama Emirates, Qatar, Ethiopia Airways na Kenya Airways yanayosafirisha mizigo na abiria kupitia kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyere ambapo katika kipindi cha Julai hadi Aprili mwaka huu shirika limebeba tani 2893.

Send this to a friend