Serikali yavuka lengo la makusanyo ya mapato ya ‘betting’

0
22

Serikali imefanikiwa kuvuka lengo katika makusanyo ya michezo ya kubashiri ambapo kufikia mwezi Mei mwaka huu imekusanya TZS bilioni 146.9 na ambapo lengo lilikuwa kukusanya TZS bilioni 131.5.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Kinondoni, Tarimba Abbas alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa Fedha 2023/24 iliyowasilishwa leo bungeni jijini Dodoma.

Kutokana na mafanikio yanayotokana na michezo ya kubahatisha, Tarimba ameishauri Serikali kuwa michezo hiyo iwe chini ya wizara ya michezo ili fedha hizo zipelekwe kwenye wizara hiyo.

“Yawezekana tumechelewa lakini Serikali ilichukue suala hili michezo hii ipelekwe chini ya wizara ili fedha zote hizi zipelekwe kwenye michezo. Huwezi kuwa na kitu kinachozalisha bilioni 146 na hadi Juni watafika bilioni 170 halafu ukawape bilioni  35 [bajeti],” amesema.

Ameeleza hayo akikosoa bajeti ya wizara hiyo ambayo ni TZS bilioni 35, kiwango ambacho wabunge wengi waliochangia wamesema ni kiwango kidogo sana.

Send this to a friend