Tanzania yakusanya bilioni 70 kwa ndege zinazotumia anga lake

0
26

Tanzania imekusanya zaidi ya TZS bilioni 70 kwa mwaka wa fedha 2022/23 (hadi sasa) ikiwa ni mapato yanayotokana na ndege zinazotumia anga lake.

Akizungumza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete katika mkutano wa wadau wa uongozaji ndege uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam amesema makusanyo hayo ni matokeo ya maboresho ya teknolojia yaliyoifanya nchi kuwa na uwezo wa kuona ndege yoyote inayopita katika anga la Tanzania.

CAG Zanzibar aliomba radhi Baraza la Wawakilishi kwa kutoa kauli ya ‘kulibeza’

“Kwa sasa hakuna ndege inayopita katika anga la Tanzania isionekane, na naipongeza Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kwa kuongeza makusanyo,” amesema.

Ameongeza kuwa kabla ya teknolojia hizo, Tanzania ilikuwa ikipata TZS bilioni 24 pekee mwaka 2014 kutokana na ndege zinazotumia anga lake hivyo, kupitia teknoloja hiyo kufikia mwaka huu wa fedha takribani TZS bilioni 83 zitakusanywa.

Send this to a friend