Singida Big Stars yauzwa kwa Fountain Gate

0
39

Uongozi wa Singida Big Stars umefanya maamuzi ya kuiuza timu hiyo kwa wamiliki wa Fountain Gate ambapo sasa timu hiyo imebadilishwa jina na kuwa “Singida Fountain Gate Footbal Club.”

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Singida Big Stars ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Bodi ya Singida Fountain Gate, John Kadutu amesema sababu ya kuiuza timu hiyo kwa Fountain Gate ni kutokana na changamoto mbalimbali za uendeshaji pamoja na nia ya kutaka kuipeleka mbali zaidi timu hiyo.

“Mnafahamu Fountain Gate wana timu nzuri ya Championship,  wana timu nzuri ya vijana wa sekondari, ni mabingwa wa Afrika. Kwahiyo tukazungumza na watu ambao wanajua nini kinatakiwa kufanyika, usimtwishe mzigo mtu ambaye hajui shida zake,” amesema.

Aidha, Kadutu amesema moja kati ya masharti makubwa waliyowapa Fountain Gate ni kwa timu hiyo kuendelea kubaki mkoani Singida pamoja na kutumia jina la Singida ili kuwaenzi wote walioisapoti timu hiyo.

Nabi: Morrison hana pumzi ya kutosha uwanjani

Naye, Rais wa Singida Fountain Gate, Japhet Makau amesema Fountain Gate imechukua asilimia 100 ya umiliki wa Singida Big Stars na Fountain Gate FC itaendelea kuwepo pia, huku akieleza kuwa hakuna tatizo lolote kwa timu hiyo kuendelea kubaki Singida kwani ilikuwa ndani ya mpango wao kufanya hivyo.

Send this to a friend