Serikali yapendekeza kufuta ada vyuo vya ufundi (DIT, MUST na ATC)

0
25

Serikali imependekeza kuondoa ada kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na kupangiwa na Serikali kujiunga na Vyuo vya Ufundi vya Dar es Salaam Institute of Technology (DIT), Mbeya University of Science and Technology (MUST) na Arusha Technical College (ATC).

Pendekezo hilo limetolewa leo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma.

Dkt. Mwigulu amesema hatua hiyo imelenga kuongeza idadi ya wataalamu wenye ujuzi na elimu inayohitajika katika zama za mapinduzi ya nne ya viwanda.

Aidha, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa ili kuhakikisha huduma za jamii zinaboreshwa na kuwezesha wananchi kushiriki katika shughuli za kuwaletea maendeleo.

Send this to a friend