Ishara 9 zinazoashiria una tatizo la afya ya akili

0
31

Kwa mujibu wa mwanasaikolojia, Hellen Mrema kutoka Pour Your Heart Psychotherapy and Counselling Centre Dar es Salaam anaeleza kuwa changamoto ya afya ya akili ni hali ya kutokuwa sawa kiakili, kisaikolojia na kihisia.

Je! Utajuaje kama unapitia tatizo la afya ya akili?

Hellen anasema kabla ya kufikia katika ugonjwa wa akili tayari mgonjwa hupitia katika changamoto ya afya ya akili ambapo mara nyingi tatizo hujionesha kupitia dalili zifuatazo;

Kukosa ufanisi
Mtu mwenye changamoto ya afya ya akili hushindwa kufanya vitu anavyopaswa na kushindwa kujihudumia mfano, kushindwa kufanya kazi ipasavyo, kushindwa kusoma.

Kuhisi wasiwasi
Sisi sote huwa na wasiwasi au ‘stress’ za mara kwa mara. Wasiwasi unaweza kuwa ishara ya ugonjwa wa afya ya akili ikiwa wasiwasi ulionao unakupata kila wakati.

Kuhisi huzuni au kutokuwa na furaha
Ikiwa hufurahii mambo uliyokuwa ukipenda awali, inaweza kuwa ishara mbaya. Kwa mfano, ikiwa ulikuwa ukifurahia kucheza mpira au kuangalia filamu lakini unahisi huna hamu ya kushiriki katika shughuli hizo kwa sasa, hiyo inaweza kuwa kiashirio kwamba afya yako ya akili haiko sawa.

Mazoea haya ya kila siku yanaweza kuharibu figo zako

Mlipuko wa kihisia
Kila mtu ana hisia tofauti, lakini mabadiliko ya ghafla na makubwa ya hisia kama vile hasira, inaweza kuwa dalili ya ugonjwa wa akili.

Matatizo ya usingizi
kukosa usingizi, kulala sana au kidogo sana kunaweza kuwa ishara hatari.

Kujitenga
Kukataa kujiunga katika shughuli za kijamii na kutochangamana na wengine kunaweza kuwa ishara ya kuhitaji msaada.

Kujisikia hatia au kuhisi huna thamani
Mawazo kama vile ‘hakuna anayenijali, ‘ni kosa langu’ au ‘sina thamani’ yote ni dalili zinazowezekana za ugonjwa wa akili. Wakati mwingine mtu anaweza kuonesha hisia ya kujiumiza au kujiua, hii humaanisha anahitaji msaada.

Dalili mbaya za kimwili;

Dalili hizo ni kama kutokwa na jasho, mapigo ya moyo ya haraka, kizunguzungu na maumivu ya kichwa.

Send this to a friend