TFF kuwaongezea adhabu wanaojihusisha na mpira licha ya kufungiwa

0
21

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema ni kosa kushirikiana na wadau wa mpira wa miguu ambao tayari wamefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira.

Katika taarifa iliyotolewa ambayo haijataja wahusika waliofungiwa, TFF imesema ni muhimu kuzingatia kuwa wadau husika wamefungiwa baada ya kwenda kinyume na katiba, kanuni na taratibu zinazosimamia mpira wa miguu.

Nabi: Morrison hana pumzi ya kutosha uwanjani

“Waliofungiwa wanajiweka katika hatari ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu iwapo hawatatumikia adhabu zao kikamiliffu,” imesema taarifa ya TFF.

TFF imesema inaendelea na kufuatilia ukiukwaji huo ili kuchukua hatua stahiki.

Send this to a friend