Asilimia 82 ya madereva Kenya wafeli mtihani wa udereva

0
34

Baada ya agizo la Waziri wa Uchukuzi,  Kipchumba Murkomen la kufanyika kwa majaribio ya lazima kwa madereva wa magari ya utumishi wa umma wanaotaka kurejesha leseni zao yanayosimamiwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA) nchini Kenya,  takwimu zimeonesha madereva wengi wamefeli majaribio hayo.

Akiwasilisha matokeo hayo, Mkurugenzi na Mkuu wa Uzingatiaji Usalama, Wilson Tuigong amesema kati ya madereva 302 waliojaribiwa kati ya Juni 9 na siku ya Ijumaa iliyopita, ni madereva 54 tu waliofaulu sawa na asilimia 18 tu.

“Hii inaonyesha kuwa kiwango cha ufaulu ni asilimia 18, jambo ambalo tunalihusisha zaidi na kukosekana kwa mitaala ya udereva kwa muda mrefu nchini kote na leseni zilizokuwa zikipatikana kwa urahisi hapo awali, jambo ambalo lilitoa mwanya kwa madereva wasio na sifa kuzipata.

Wananchi Kigoma wafunga barabara kushinikiza ramli ili kufukuza wachawi

Mwaka wa 2018, tulikuja na sheria na mtaala ambao ungesawazisha mafunzo ya udereva, lakini ukakataliwa na Bunge. Tulianza mchakato huo tena mnamo 2019 na mnamo Machi 10, 2020, sheria zilitangazwa kwenye gazeti la serikali,” amesema Tuigong.

Ameeleza kuwa baadhi ya wale ambao hawakufaulu mtihani wa udereva walikuwa na matatizo ya kutambua alama za barabarani kutoka kwenye michoro iliyotundikwa kwenye kuta za vyumba vya mitihani, huku wengine wakishindwa kueleza jinsi ya kufuata kanuni mbalimbali za barabarani.

Kujaribiwa kwa madereva wa magari ya kibiashara na ya huduma za umma ni mkakati mpya wa utoaji wa leseni za madaraja B3, D1, D3, C, C1.CE na CD, ambazo hujumuisha mabasi, magari aina ya matatu yenye viti 14, mabasi ya shule na teksi.

Send this to a friend