LATRA: Hatuwatambui madereva waliosababisha ajali za mabasi ya New Force

0
32

Kufuatia wimbi la ajali lililoikumba kampuni ya mabasi ya New Force, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imesitisha ratiba za mabasi 38 ya Kampuni hiyo yanayoanza safari kuanzia saa 9:00 na saa 11 alfajiri.

Akizungumza Mkurugenzi wa LATRA, Habibu Saluo amesema mamlaka ilifanya uchunguzi na kubaini kuna uvunjaji wa sheria kwa makusudi uliyopelekea ajali za mabasi matano ya abiria ndani ya wiki nne na kusababisha madhara ikiwemo vifo vya abiria.

“Kufuatia ukiukwaji huu na mfulululizo wa matukio ya ajali kwenye kampuni ya New Force, Mamlaka inafuta ratiba za saa 9.00 alfajiri na saa 11.00 alfajiri kwa mabasi yote 38 ya New Force Enteprises, ambapo mabasi 10 ni yale yanayoanza safari saa 9.00 alfajiri na mabasi 28 yanayoanza safari saa 11.00 alfajiri. Hivyo, kuanzia tarehe 5 Julai, 2023, mabasi haya yatafanya safari zao kuanzia saa 12.00 asubuhi na kuendelea,” imesema LATRA.

Aidha, mamlaka imesema imeshindwa kuwatambua madereva waliokuwa wanaendesha mabasi hayo ili kuweza kuwachukulia hatua au kupeleka taarifa zao Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani ili wawajibishwe kutokana na madereva hao kutotambulika na LATRA.

Send this to a friend