Mfanyabiashara, Rostam Aziz amekiomba radhi Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) kufuatia kauli yake aliyoitoa dhidi ya Mahakama nchini saa chache baada ya chama hicho kumtaka athibitishe kauli yake aliyoitoa dhidi ya mahakama.
Rostam amesema kuwa ni kuteleza kwa ulimi lakini dhamira yake haikuwa kutamka maneno hayo na badala yake ilikuwa ni kuuelimisha umma juu ya uwekezaji na namna ambavyo inabidi ufanyike kwenye nchi husika.
“Ningependa kuuhakikishia umma, kwamba wakati nikizungumzia kuhusu uwekezaji halikuwa kusudio langu kudharau Mahakama zetu kama nilifanya hivyo ilikuwa ni kuteleza kwa ulimi,” amesema.
Juni 26, 2023 Rostam mbele ya waandishi wa habari alisema, “Hakuna mwekezaji atawekeza kwenye nchi ambayo kesi ikipelekwa hapo Kisutu kiongozi yoyote anaweza kupiga simu akaielekeza mahakama nini cha kufanya.”