Utafiti wa madaktari wa idara ya Magonjwa ya Mfumo wa Mkojo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa umebaini kuwa mitindo ya kujamiiana inaweza kusababisha uume uliosimama kwa muda mrefu kuvunjika.
Utafiti wa madaktari hao umechapishwa kwenye Jarida la kimataifa la kesi za Upasuaji (International Journal of Surgery Case Reports, 108(2023)108415) ambapo wameripoti kufanya upasuaji wa kuunga uume wa kijana mwenye umri wa miaka 27 uliovunjika wakati akijamiana na mkewe.
Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti huo, ajali ya kuvunjika uume si suala lenye kujitokeza mara kwa mara, bali linauwiano wa mtu mmoja kati ya watu 175,000.
Utafiti: Unywaji pombe wa wastani hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo
Aidha, utafiti huo unasema kuwa utafiti uliofanyika katika mataifa ya Ulaya na Marekani umeonesha kuwa asilimia 93.3 ya ajali za uume hutokana na kujamiiana, ambacho kilikuwa chanzo cha tatizo alilolipata kijana aliyetibiwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Vile vile, ajali za kuvunjika uume kwa kujichua zinashika nafasi ya pili zikiwa na asilimia 10.