Rais Samia kuwa Mgeni wa Heshima maadhimisho ya Uhuru wa Malawi

0
48

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Malawi kuanzia Julai 5 hadi Julai 7, 2023 kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais wa nchi hiyo, Dkt. Lazarus Chakwera.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi imesema katika ziara hiyo Rais Samia atashiriki katika hafla mbalimbali ikiwemo ibada ya kitaifa itakayofanyika Julai 5, maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi Julai 6, 2023 kama Mgeni Maalum wa Heshima, kutembelea moja ya eneo lililoharibiwa na Kimbunga Freddy pamoja na kufanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo.

“Ziara hiyo ya kiserikali itaunganisha uhusiano wa kati ya Malawi na Tanzania ambao tayari umeimarishwa ambao msingi wake ni uhusiano wa kihistoria, maslahi ya pande zote ili kukuza hali ya maisha ya watu wa nchi hizo mbili na maslahi ya pamoja katika ushirikiano wa kikanda na kimataifa,” imeeleza taarifa hiyo.

Rais Samia apongezwa kwa kukuza biashara na uwekezaji

Rais Samia anatarajiwa kuondoka nchini humo siku ya Ijumaa Julai 07, 2023 kupitia uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chileka.

Ushirikiano kati ya Tanzani na nchi ya Malawi umeendelea kuimarika hasa katika sekta ya uchumi na biashara, ambapo mwaka 2022 Malawi ilipitisha mizigo tani 557,826 kupitia Bandari ya Dar es Salaam, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.3 kutoka tani 471,385 mwaka 2021.

Send this to a friend