Watu milioni 10 wajiunga Threads ndani ya saa 7, yaahidi kuipita Twitter
Watumiaji milioni 10 wamejisajili kwenye programu tumizi ya ‘Threads’ iliyozinduliwa na kampuni ya Meta katika kipindi cha saa saba tangu kuzinduliwa kwake.
Mmiliki wake, Mark Zuckerberg amesema programu hiyo inalenga kuushinda mtandao wa Twitter, huku wataalam wakidai Threads inaweza kuwavutia watumiaji wengi wa twitter ambao hawafurahishwi na mabadiliko ya hivi karibuni katika mtandao huo.
“Itachukua muda [kuipita twitter], lakini nadhani kuwe na programu ya mazungumzo ya umma yenye watu bilioni 1+ ndani yake. Twitter imepata fursa ya kufanya hivi lakini haijahimili. Tunatumaini tutafanya hivyo,” amesema Mark Zuckerberg.
Sasa utaweza kuhariri (edit) ujumbe unaotuma WhatsApp
Threads ambayo haijazinduliwa katika Umoja wa Ulaya kwa sasa inaruhusu watumiaji kuchapisha hadi herufi 500, huku ikiwa na ina vipengele vingi sawa na Twitter.
Kwa sasa program hiyo inapatikana katika zaidi ya nchi 100 ikiwemo Uingereza, huku tayari ikiwa na watu mashuhuri kama Jennifer Lopez, Shakira na Hugh Jackman, pamoja na vyombo vya habari vikiwemo The Washington Post na The Economist.