Polisi nchini Kenya wamelazimika kupiga mabomu ya machozi kutawanya kundi la wanaharakati wa haki za binadamu akiwemo Jaji Mkuu Mstaafu, Willy Mutunga baada ya kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Nairobi, akitaka kuachiliwa huru kwa waandamanaji waliokamatwa.
Jaji na wanaharakati walienda kituoni hapo wakitaka kuachiliwa mara moja kwa zaidi ya watu 30 waliokamatwa wakati wa maandamano siku ya Sabazaba ambayo yaliongozwa na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga.
Balozi Karume afutwa uanachama CCM
Imeelezwa kuwa Jaji Mutunga ameshirikiana na wanaharakati na wanasheria akiwemo Kamishna wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya Victor Kamau na Wakili Lempaa Soyinka ambao waliweka kambi kituoni hapo kutaka kuachiliwa bila masharti kwa waandamanaji hao.
Odinga aliitisha mkutano katika uwanja wa Kamukunji na kuanzisha maandamano yaliyolenga kushinikiza Rais William Ruto na serikali yake kuondoka madarakani kwa madai mbalimbali ikiwemo kupanda kwa gharama za maisha nchini humo.