Serikali Zanzibar yatoa ufafanuzi suala la wanaume kusuka

0
13

Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar limefafanua kuwa mwanaume yeyote atakayekamatwa akiwa amesuka adhabu yake ni kulipa faini ya shilingi milioni 1 au kifungo cha miezi sita jela au vyote kwa pamoja.

Akizungumza na Swahili Times, Katibu Mtendaji baraza hilo, Dkt. Omar Adam amesema kwa mujibu wa utaratibu wa mila na desturi za Zanzibar mtoto wa kiume haruhusiwi kusuka nywele za aina yoyote, na sheria inakataza mtu yeyote kukiuka mila na desturi zilizopo.

Kuhusu watalii wanaofika visiwani humo ikiwa watawajibika na utaratibu wa ulipaji faini, amesema faini hiyo inawahusu watu wote walio ndani na wageni kutoka nje ya Zanzibar.

“Duniani hakuna mipaka ya sheria, Uchina ukikamatwa na unga maana yake hukumu yako ni kifo, haijalishi umetoka wapi, kwa hiyo na hii ni sheria ipo Zanzibar kwa watu wote waliokuwepo kwenye mipaka ya Zanzibar.

MOI yalaani kitendo cha mgonjwa ‘kubusiana’ wodini

Lakini utafiti tulioufanya katika wageni 1,000 hakuna hata mmoja aliyesuka, watu wengi wanaosuka ni kutoka Zanzibar na kutoka Tanzania Bara na maeneo ya mwambao ya Pwani ya Mashariki. Haitakuwa na maana yoyote wageni wanakuja wanasuka halafu wanawaambukiza vijana wetu, wanawaacha katika mazingira ambayo sio salama na sio sahii,” amesema Dkt. Omar.

Aidha, amesema mpaka sasa tayari kuna watu waliokamatwa na kupewa onyo kwa kunyolewa nywele zao, na kueleza kwamba watakaokamatwa kuanzia sasa watalipa faini, na ikiwa kosa hilo litajirudia watawajibika kutumikia kifungo.

Send this to a friend