Ripoti: Tanzania yashika nafasi ya 17 kwa nchi zenye amani Afrika

0
32

Ripoti mpya ya Taasisi ya Uchumi na Amani (IEP) ya mwaka 2023 toleo la 17 imetoa takwimu ya nchi zenye amani zaidi barani Afrika ambapo utafiti huo unaonesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 17 kwa amani na kushika nafasi ya 91 kidunia.

IEP imesema Tanzania imeshika nafasi hiyo kwa kupata alama 2.058 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Mauritius kwa kupata alama 1.546, kidunia ikishika namba 23. Nchi ya pili ni Botswana ambayo imepata alama 1.762 huku kidunia ikishika namba 42.

Katika ripoti ya taasisi hiyo ya mwaka 2022, Tanzania ilikuwa nafasi ya 16 ikiwa na alama 2.001 na 86 kidunia.

Nchi 10 ambazo watu wake wanaongoza kupata ‘depression’

Aidha, nchi za mwisho kidunia ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyoshika nafasi ya 159, ikifuatiwa na Sudan Kusini nafasi ya 160, Syria nafasi ya 161, Yemen 162, kisha nchi iliyoshika mkia kidunia ni Afghanistan ikiwa ya 163.

Ripoti imetaja sababu za kuzorota kwa amani kuwa ni migogoro, vifo kutokana na migogoro ya ndani, mahusiano ya nje na nchi jirani, kukosekana kwa utulivu wa kisiasa na migogoro mingine hasa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia.

Send this to a friend