Wakili Madeleka akamatwa Arusha

0
24

Wakili wa kujitegemea nchini, Peter Madeleka amekamatwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Jumuishi cha utoaji haki baada ya kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Wakili huyo aliwasilisha maombi namba 80 ya mwaka 2021 kutokana na kesi aliyokuwa amefunguliwa ya uhujumu uchumi namba 40/2020.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi iliyotolea uamuzi Aprili 27 mwaka huu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, wakili Madeleka alikuhukumiwa kulipa faini ya TZS laki 2 au kutumikia kifungo cha nje cha miaka mitatu, pia alilipa shilingi milioni 2 kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ili kuondolewa shauri hilo baada ya kulazimika kukiri makosa.

Hata hivyo wakili huyo alifungua kesi Mahakama Kuu, kupinga uamuzi wa Hakimu Mkazi Arusha kumtia hatiani katika kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, pia aliiomba Mahakama Kuu itoe amri ya kurejeshewa faini ya TZS laki 2 aliyolipa kwa sababu mchakato mzima ulikuwa ni kinyume cha sheria.

Wakili Madeleka amedai baada ya hukumu hiyo, alilazimishwa kufanya makubaliano ya kukiri kosa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) na baada ya kuachiwa alikata rufaa.

Akizungumzia kuhusu kukamatwa kwa mteja wake, Wakili Simon Mbwambo amesema hajui kosa analokabiliwa nalo wakili Madeleka.

“Sijui kosa naona polisi wamemkata na wanampeleka Ofisi ya RCO (Mkuu wa Upelelezi Mkoa Arusha) kwa mahojiano, labda wanataka kuanza upya kusikiliza kesi hii ya leo,” amesema.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend