Ndege za ATCL hatarini kukamatwa

0
16

Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kimeiamuru Tanzania kulipa dola milioni 109.5 [TZS bilioni 266] kwa kampuni za uchimbaji madini zilizosajiliwa Uingereza, Ntaka Nickel Holdings Ltd na Nachingwea UK Ltd, kufuatia uamuzi uliochukuliwa wakati wa utawala wa Hayati Rais Dkt. John Magufuli mwaka 2018 wa kufuta leseni yao ya uchimbaji wa madini ya nikeli.

Kampuni hizo zilifungua kesi na kufanikiwa kuishinda Tanzania katika mahakama ya Benki ya Dunia kwa kukiuka wajibu wake chini ya Mkataba wa Uwekezaji wa Pamoja (BIT) kati ya Uingereza na Tanzania na sheria za kimataifa kwa kutaifisha leseni hiyo.

Tanzania pia imeamriwa kulipa dola milioni 3.859 [TZS bilioni 9.3] kama gharama za kisheria kwa walalamikaji, pamoja na ada na gharama za ICSID.

Kampuni ya Australia, Indiana Resources Ltd ambayo ni mmiliki mkuu wa mradi wa nikeli wa Ntaka, hapo awali ilionya kuwa itachukua ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL). Indiana sasa inasema itachukua hatua haraka kutekeleza uamuzi wa mahakama.

EWURA: Nchi ina mafuta ya kutosha, yawaonya wanaoficha

Kampuni za EcoDevelopment na EcoEnergy za Sweden mwaka jana zilishinda kesi ya dola $165m [TZS bilioni 401] dhidi ya Tanzania kwenye ICSID kufuatia uamuzi wa Serikali ya Magufuli kuwanyang’anya wawekezaji hao ardhi ya Bagamoyo, kinyume na Mkataba wa Uwekezaji wa Pamoja (BIT) kati ya Sweden na Tanzania.

Kampuni hizo zilikamata ndege ya Airbus inayomilikiwa na Wakala wa Serikali wa Ndege za Serikali (TGFA) inayoendeshwa na ATCL ili kutekeleza hukumu ya ICSID, hata hivyo ndege hiyo yenye namba za usajili 5H-TCH hivi karibuni ilirejea Tanzania baada ya serikali kumaliza kesi hiyo.

Send this to a friend