Rais Samia amzawadia milioni 2 mwanamke anayejitolea kuwakumbatia watoto njiti

0
15

Rais Samia Suluhu Hassan amemzawadia TZS milioni 2 Mariam Mwakabungu (25) mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam kutokana na kujitolea kwake kutunza watoto waliozaliwa kabla ya wakati.

Mama huyo amekuwa gumzo mitandaoni kwa takribani siku mbili baada ya kujitolea kuwakumbatia watoto hao na kuwapatia joto lake katika Hospitali ya Amana.

Rais Samia ametuma ujumbe huo leo Julai 19, 2023 uliowasilishwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Brayson Kiwelu ambaye amemkabidhi Mariam kiasi hicho cha fedha.

“Nawashukuru kwa kupokea vizuri taarifa hii kuhusiana na mama yetu huyu ambaye amekuwa akijitoa kwa ajili ya kuwahudumia hawa watoto njiti na ambao wametelekezwa na mama zao au wale ambao wamepoteza mama zao kwa sababu mbalimbali.

Utafiti mpya: Unywaji pombe wa wastani hupunguza hatari yamagonjwa ya moyo

Rais Samia Suluhu Hassan ambaye wakati wote amesema kipaumbele chake yeye ni afya hasa kwenye kitengo cha afya ya mama na mtoto, kwa kuguswa huko amelazimika kutuma mkono wa asante na pongezi kwa mama huyu, kumtia moyo kwa kazi nzuri aliyoifanya na ametupa kiasi cha TZS milioni 2 ikiwa ni sehemu ya shukrani yake,” amesema.

Ameongeza kuwa “Rais Samia ameshukuru sana msaada ambao mama huyo ameutoa na amewataka Watanzania kuendelea kujitoa kwa ajili ya kuhudumia wale wenye uhitaji.”

Send this to a friend