Baada ya kupungua kwa janga la UVIKO-19, ubora wa maisha unaongezeka tena katika miji mingi duniani. Kwa mujibu wa kielelezo cha kila mwaka cha Annual Global Liveability Index, ambacho kinafuatilia na kupanga ubora wa miji 173 kimezingatia vigezo kadhaa vikiwemo huduma za afya, utamaduni, usalama, mazingira, elimu na miundombinu.
Hii ni orodha ya majiji mazuri duniani ya kuishi kwa mwaka 2023;
1.Vienna, Austria
Mji mkuu wa Austria, Vienna sio mgeni kwenye kushika namba moja katika orodha ya kila mwaka ya majiji bora ya kuishi kwa mujibu wa Annual Global Liveability Index, ikiwa na vigezo vya ubora vilivyokamilika kama huduma za afya, elimu na miundombinu.
Mfumo wa usafiri wa umma ni wa uhakika, huduma za utunzaji watoto ni nafuu na urahisi wa kuifikia migahawa na majumba ya sinema lakini pia ina aina mbalimbali za majengo ya kihistoria ya kuvutia.
2.Melbourne, Australia
Melbourne ina eneo la ajabu la chakula, sanaa za kitamaduni, matukio na vivutio, na vile vile michezo na matukio yote makubwa ya kimataifa. Kwa mujibu wa wakazi, katika jiji hilo ni rahisi kusafiri, kwa usafiri bora unaokufikisha mpaka kwenye vitongoji. Pia inachukua muda mfupi kufika kwenye fukwe maarufu na maeneo ya mvinyo.
3.Vancouver, Canada
Miji mitatu ya Canada (ikiwa ni pamoja na Calgary na Toronto) imeingia katika 10 bora mwaka huu, lakini Vancouver iliorodheshwa ya juu zaidi (nafasi ya tano) kutokana na sifa yake.
Vancouver iko pwani ya magharibi mwa Canada na ni mojawapo ya majiji ya kuvutia zaidi duniani. Ina mandhari nzuri ya milima na bahari, pia ni maarufu kwa utamaduni wake, chakula kizuri, na mazingira safi.
4.Osaka, Japan
Osaka imeorodheshwa katika 10 bora, na Japan ndio nchi pekee ya Asia iliyoingia kwenye orodha hiyo.
Osaka ni mji wenye utamaduni, vyakula vya kuvutia, na maisha ya kisasa. Inajulikana kama “Jiji la Mapishi” na ina vivutio vingi vya utalii kama vile Osaka Castle na Universal Studios Japan. Pamoja na fukwe nzuri na maeneo ya kijani, Osaka inatoa mazingira mazuri ya kuishi yenye gharama nafuu.
5.Auckland, New Zealand
Mji mkubwa na mji mkuu wa New Zealand. Unajulikana kwa mandhari yake nzuri, visiwa, na fukwe nzuri. Auckland pia huchukuliwa kama mojawapo ya miji salama na yenye amani duniani.