Bia iliyotengenezwa kutokana na maji machafu ya kuogea

0
27

Epic OneWater Brew, ni bia iliyotengenezwa na kampuni ya Epic Cleantec na kiwanda cha bia cha Devil’s Canyon, ambayo imetokana na maji machafu yaliyotumika kutoka kwenye vyumba vya kuogea, kufulia na visinki vya bafuni katika jengo lenye ghorofa 40 huko San Francisco.

Kampuni hiyo ya Epic ina vifaa maalum vya kufuatilia, kutibu na kutumia maji kwa ajili ya matumizi ambapo imebainisha kuwa, bia hiyo ni salama kabisa kwa kunywa.

Huwezi kupata bia hii sokoni kwa hivi karibuni. Epic imeweka wazi kuwa ni bidhaa ya maonesho na lengo la kampuni hiyo ni kuwafanya watu watambue kuhusu uwezekano wa kuzalisha tena maji yaliyotumika kama biashara.

“Tulitaka kufanya kitu kizuri ambacho kingewavutia watu na kuwafanya wawe na msisimko, lakini pia kuonyesha uwezo usiotumika vizuri tena kwa kutumia maji,” amesema Aaron Tartakovsky, mwanzilishi mwenza na Afisa Mkuu Mtendaji wa Epic Cleantec.

Epic Cleantec inaweka vifaa vyake katika majengo kwa ajili ya kuzalisha tena maji, hivyo kuepuka kuyatiririsha majitaka kwenye mfereji, huyapeleka kwenye kituo cha matibabu. Kampuni hiyo inatumia hadi asilimia 95 ya majitaka, iwe maji meusi yanayotokana na vyoo au maji meupe yanayotokana na visinki, mashine za kufulia, na mabafu.

Kenya: Wanawake wanawalipa wanaume milioni 5 wawape mimba

Ingawa mfumo wa Epic Cleantec hauna lengo la kuzalisha maji kwa ajili ya kunywa, sheria za sasa zinaruhusu matumizi tena ya maji machafu katika majimbo mengi ya Marekani, ikiwa ni pamoja na California na Texas. Majimbo kama Arizona, Colorado, Florida, New Mexico, na Washington, yapo katika mchakato wa kuboresha sheria zao za matumizi tena ya maji.

Send this to a friend