Mtanzania atekwa Nigeria, wataka milioni 170 kumuachia huru

0
16

Frateri Mtanzania atekwa Nigeria, wataka milioni 170 kumuachia huru
Frateri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma, Melkiori Mahinini (27) ametekwa nyara na watu wasiojulikana nchini Nigeria alikopelekwa na Shirika la Wamisionari wa Afrika kwa ajili ya mwaka wa uchungaji kabla ya kuanza masomo ya teolojia.

Taarifa iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Kigoma, Joseph Mlola inadai frateri huyo alikamatwa Agosti 4 mwaka huu katika jimbo la Minna huko Nigeria akiwa na mwenzake ambaye ni raia wa Burkina Faso, Padri Paul Sanogo.

Akizungumza Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dk Benson Bana amekiri kuwepo kwa tukio hilo, na kwamba wanachukua hatua mbalimbali kuhakikisha Mtanzania huyo pamoja na mwenzake wanaachiwa huru.

Kenya: Makaburi yagundulika kanisani, mapya yaibuka

Ameongeza kuwa watekaji wameamuru wapewe Naira milioni 100 (sawa na TZS milioni 325.1) ili kuwaachia huru wote wawili, hivyo kila mmoja anatakiwa kulipiwa karibu Dola 70,000 za Marekani ambazo ni zaidi ya TZS milioni 170 za Kitanzania.

“Tunahitaji kuwa waangalifu katika jambo hili kwa sababu watu hawa si wazuri, wakijua kwamba Serikali italipa wataongeza dau hadi Naira 500 milioni. Kwa hiyo, tunaendelea kushirikiana na wenzetu wa Shirika la Wamissionari wa Afrika ambao tayari wametoa taarifa polisi,” alisema.
Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend