Benki ya Dunia yasitisha mikopo kwa Uganda kutokana na sheria ya kuzuia mapenzi ya jinsia moja

0
44

Benki ya Dunia imetangaza kusitisha mikopo kwa ajili ya miradi nchini Uganda kwa siku zijazo kutokana na nchi hiyo kupitisha sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja jambo lililotajwa kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Taarifa kutoka kwa benki hiyo imesema ufadhili huo umesitishwa hadi mamlaka nchini Uganda itakapotoa sera ya kuwalinda watu hao wakiwemo wasagaji, mashoga, watu wa jinsia mbili, waliobadili jinsia na makundi mengine ambayo kwa kawaida yanaainishwa kama LGBTQ+.

Benki imesema sheria hiyo inayoharamisha LGBTQ iliyopitishwa miezi michache iliyopita inakwenda kinyume na misingi na maadili ya Benki ya Dunia ambayo haibagui yeyote kwa misingi ya jinsia au rangi yake katika azma yake ya kutokomeza umasikini duniani.

Kenya: Makaburi yagundulika kanisani, mapya yaibuka

Sheria hiyo mpya ambayo Rais Yoweri Museveni aliisaini mwezi Mei inatoa adhabu kali ikiwemo hukumu ya kifo, jambo lililoleta upinzani mkubwa kutoka kwa makundi ya haki za binadamu na nchi za Magharibi, ikiwa ni pamoja na Marekani ambayo ni mdhamini mkubwa wa Benki ya Dunia.

Uganda imekuwa na msimamo mkali na wa wazi dhidi ya mapenzi ya jinsi moja, ikiyataja mapenzi ya jinsia moja kama kinyume na maadili ya utamaduni wa nchi hiyo.

Send this to a friend