Nyota wa Brazil, Neymar (31) amekubali mkataba wa miaka miwili wa kujiunga na klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia na kuachana na klabu yake ya Ufaransa, Paris Saint-Germain (PSG).
Neymar anafanyiwa vipimo vya afya leo na anatarajiwa kukamilisha hatua hiyo ndani ya saa 48 zijazo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky Sports News, klabu ya PSG iko tayari kupokea hadi £86.3m [TZS bilioni 274.64] kwa mchezaji huyo raia wa Brazil kutoka klabu ya Al Hilal.
PSG ilipanda dau na kuvunja rekodi ya dunia mwaka 2017 ilipofanya uhamisho wa Neymar kutoka Barcelona kwa £200m [TZS bilioni 636].
Mishahara inayotolewa na vilabu vya Saudi Arabia mara nyingi huwa juu zaidi kuliko ile ambayo wachezaji wanaweza kupata katika ligi za Ulaya na kulingana na Sky Sports News, Neymar atapokea (£129.2m [TZS bilioni 410.93] kwa mwaka mara sita ya kiasi alichopata PSG.