Kampuni ya Sola Yazindua Kampeni ya Matumizi ya Nishati Safi

0
20

Katika kampeni ya kuunga mkono jitihada za serikali kwenye matumizi nishati salama kimazingira, kampuni ya sola d.light Tanzania Limited imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi huku wateja wake pia watapata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali pale watakapolipa mikopo yao iliyosalia au kwa wakati.

Kampeni hiyo mpya ambayo inajulikana kama ‘Mwanga Wako, Mchongo Wako’ itawapatia fursa wateja wenye bahati kujishindia zawadi mbalimbali kama vile mfumo wa nishati ya jua kwa matumizi ya nyumbani watakapolipa siku 90 kwa mkupuo; baiskeli watakapolipa kila siku; simu janja za Infinix Smart 6 4G watakapolipa siku 60 kwa mkupuo; Nokia C2 watakapolipa siku 30 kwa mkupuo, na vifurushi vya muda wa maongezi vya shilingi 20,000 wakimaliza malimbikizo ya mikopo yao.

Baadhi ya zawadi zinazotolewa na kampuni hio kwenye kampeni ya Mwanga Wako, Mchongo Wako.

Thamani ya zawadi zitakazotolewa katika kampeni hii zitakuwa na jumla ya thamani ya shilingi milioni 11 za Kitanzania na kampeni hio inatarajiwa kuanza tarehe 14 Agosti kwa muda wa miezi miwili, itajumuisha mikoa ambayo ina matumizi makubwa ya nishati ya jua ikiwemo Arusha, Dar es salaam, Geita, Iringa,  Katavi, Kilimanjaro, na Lindi.

Meneja huduma kwa wateja, Sarah Sonelo akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye uzinduzi wa kampeni hio jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa d.light Tanzania Limited, Bw. Charles Natai amesema kuwa lengo kubwa la kampeni hii ni kuhamasisha watanzania kutumia nishati safi ya sola ili kuleta mapinduzi ya matumizi ya nishati ya jua nchini badala ya nishati zinazohatarisha mazingira na tabaka la Ozoni.

“Kampeni hii inalenga kuwapa hamasa wateja kuhamia kwenye nishati safi na sisi kama d.light tumeona ni vyema kutambua mchango wa kila mteja wa kweli. Hivyo basi, tunapenda kuwataarifu kuwa tutakuwa tunawazadia kila mwisho wa mwezi, hii ni kwa wateja wetu wa sasa ambao bado hawajarudisha mikopo yao au kulipa kwa wakati, lakini pia kwa wateja wapya watakaojiunga nasi. Kama hiyo haitoshi, kutakuwa na zawadi kubwa mwishoni mwa kampeni hii ambapo tutawatangazia Watanzania,” aliongezea Bw. Natai.

Mkurugenzi Mkuu wa d.light Tanzania, Charles Natai akizindua zawadi ya kampeni yao iitwayo ‘Mwango Wako, Mchongo Wako’ inayolenga kuhamasisha watu kwenye matumizi ya nishati safi ya jua nchini ambapo wateja watajishindia zawadi mbalimbali kwa kipindi cha miezi miwili. Kampeni hio imezinduliwa rasmi tarehe 15 Agosti mjini Arusha na italenga mikoa yote ya Tanzania.

Kwa upande wake Madinda Juma ambae ni miongoni mwa wakala wa d.light alisema, ‘tangia nimeanza kununua bidhaa za d.light mwaka 2020, imenisaidia sana kukua kimaisha, nimetoka kipato cha chini sana hadi leo niko kipato cha kati. Pamoja na yote, nimeweza kujenga nyumba yangu.’

Mkurugenzi Mkuu wa d.light Tanzania, Charle Natai akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hio kwenye uzinduzi wa kampeni hio.

Kampuni hio tayari imewasadia watu zaidi ya milioni 100 barani Afrika na watu wapatao laki mbili nchini Tanzania katika matumizi ya nishati safi ya sola.

 

Send this to a friend