Mfumuko wa bei umekuwa ukitia shaka katika uchumi wa nchi kadhaa za Afrika, na hivyo kuwa changamoto kwa serikali, biashara, na wananchi kwa ujumla. Bara hili limekabiliana na viwango tofauti vya mfumuko wa bei, ambavyo vimeathiri uwezo wa wanunuzi, utulivu wa kiuchumi, na mengineyo.
Idadi ya mataifa ya Afrika yamepitia kipindi kirefu cha mfumuko mkubwa wa bei, ambao unapunguza thamani halisi ya pesa. Sababu zinazochangia changamoto hii ni nyingi ikiwemo kuvurugika kwa ugavi wa bidhaa, kupungua kwa thamani ya sarafu, kutokuwa na utulivu kisiasa, miundombinu duni, na kutofautiana kwa bei za bidhaa kimataifa.
Orodha hii imetolewa kwa hisani ya Trading Economics, jukwaa la data ambalo hutoa data sahihi kwa nchi 196, ikiwa ni pamoja na data za kihistoria na makadirio kwa zaidi ya viashiria vya uchumi milioni 20, viwango vya sarafu, hesabu za masoko ya hisa, faida za dhamana za serikali, na bei za bidhaa.
Hizi ni orodha za nchi 10 za Afrika zenye kiwango cha juu cha mfumuko wa bei katikati mwa mwaka 2023;
1.Zimbabwe:101%
2.Sierra Leone: 44.81%
3.Ghana:43.1%
4.Misri: 36.5%
5.Ethiopia:28.8%
6.Malawi:27.3%
7.Nigeria:24.08%
8.Gambia:17.81%
9.Rwanda:17.3%
10.Angola:12.12%
Kwa Tanzania mfumuko wa bei kwa Julai 2023 ulikuwa asilimia 3.3, ikiwa ni moja ya nchi chache za Afrika zenye kiwango cha chini zaidi cha mfumuko wa bei.
Chanzo: Business Insider