Mtoto Hamimu aliyekuwa na matatizo ya ngozi akabidhiwa nyumba na Rais Samia

0
24

Mtoto Hamimu Baranyikwa aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ngozi amekabidhiwa rasmi nyumba aliyojengewa na Rais Samia Suluhu Hassan katika Kijiji cha Nyakanazi, Kata ya Rusahunga Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.

Akimkabidhi nyumba hiyo kwa niaba ya Rais Samia, Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Advera Bulimba amesema nyumba hiyo ni ahadi ya Rais Samia ambayo aliitoa Oktoba 2022 wakati wa ziara yake wilayani humo baada ya kumkuta akiwa katika hali mbaya.

“Mheshimiwa Rais alitoa ahadi hiyo kwa huyu mtoto ambaye alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya ngozi. Mheshimiwa Rais ameniagiza mimi ACP. Advera John Bulimba, Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo niweze kuikabidhi nyumba hiyo kwa mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa kwa niaba yake,” amesema.

JWTZ yamsaka aliyesambaza uzushi mitandaoni

Rais Samia Suluhu alimweona kwa mara ya kwanza mtoto huyo kwenye msafara wake akiwa kwenye ziara mkoani Kagera, akiwa amekaa kwa huzuni pembezoni mwa barabara na ngozi yake ikiwa imeharibika vibaya.

Hata hivyo, Rais aliguswa na kugharamia matibabu yake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alikaa kwa takribani miezi sita mpaka aliporuhusiwa kwenda nyumbani Aprili 19, mwaka huu.

Send this to a friend